Friday, May 10, 2013

FURAHA ZATAWALA BAADA YA KUACHIWA KWA SHEIKH PONDA ISSA PONDA HAPO JANA...ALHAMDULILLAH!

Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu TanzaniaSheikh Ponda Issa Ponda pamoja na wengine 49 walihukumiwa kifungo cha nje caha mwaka mmoja hapo jana katika mahakama ya Kisutu.
TAQBIRRRRR...ALLAH HU AKBAR!


Askari wa Magereza akimfungua pingu Katibu wa Jumuiya ya Taasisi za Kiislamu Tanzania  katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu hapo jana

Sheikh Habibu Mazinge (suti nyeusi) akimlaki Sheikh Ponda mara baada ya kuachiliwa huru.

Sheikh Ponda akizungumza na waandishi wa habari.
"Kuna utaratibu umeandaliwa na jumuiya na taasisi za kiisilamu Tanzania tutawaita tutazungumza kwa pamoja lakini kikubwa ninachoweza kusema kwamba tumeshuhudia uonevu na dhulma tunayofanyiwa waisilamu nanyie ni mashuhuda hapa leo." Alisema.Askari wakiwa kwenye msafara wa kumsindikiza Sheikh Ponda baada ya kuachiwa.

Sheikh Ponda akiswali katika Msikitini wa Mtambani pemben ni Imam Suleiman  wa msikiti wa mtamban Kinondoni B Dar es Salaam.
Taqbirrrrrrrrrr.....Allah hu Akbar!!Sheikh Ponda akihutubia katika Msikitini wa Mtambani, Kinondoni Dar es Salaam

No comments: