Monday, March 4, 2013

AJALI YA BASI YAMUUA MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA DODOMA ( UDOM )

MUNGU AILAZE ROHO YAKO MAHALA PEMA PEPONI AAMIN.


Mtu mmoja amefariki dunia papo hapo na wengine 11 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la kampuni ya Mohamed Trans likitokea Dar es salaam kwenda Dodoma baada ya kupata ajali katika eneo la Kiegea, Gairo barabara ya Morogoro-Dodoma.

Aliyefariki ametambulika kuwa ni Bernadeta Minja aliyekuwa Mhadhiri katika Kitivo cha Sayansi ya Jamii, Idara ya Uchumi na Biashara ya Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) aliyekuwa safarini na mfanyakazi wake wa ndani.

 Shughuli za msiba zinaendelea huko Kisasa, Dodoma alipokuwa akiishi marehemu.

No comments: