Tuesday, January 8, 2013

MUNGU AILAZE YA OMARI OMARI MAHALA PEMA PEPONI ...AAMIN

 

MSANII nyota wa miondoko ya Mchiriku, Omari Omari, aliyefariki leo afajiri atazikwa kesho saa 7 mchana.
Omari Omari aliyetamba na wimbo “Kupata Majaaliwa” ndani yake kukiwa na mstari mkali unaosema ndevu amekosa ng’ombe lakini mbuzi kapewa, alifariki katika hospitali kuu ya Temeke baada ya kuugua ugonjwa wa kifua kikuu.
Msiba uko Temeke Mikoroshini nyumbani kwa baba yake.
MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI.. AAMIN