Friday, January 4, 2013

MAZISHI YA SAJUKI KISUTU LEO..

MWENYEZI MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI AAMIN. WANADAMU TUKUMBUKE KUWA SOTE SAFARI YETU NI MOJA,NDUGU YETU AMETANGULIA NASI TWAFATIA  NA HAPA DUNIANI SI MAKAZI YETU YA MILELE..BASI YATUPASA TUMCHE NA TUMUOGOPE MWENYEZI MUNGU  KWA KUFANYA YALE YOTE  ALIYOYAAMRISHA NA KUACHA YALE ALIYOYAKATAZA ILI TUWE NA MWISHO ULIO MWEMA.IN SHA ALLAH

 Sehemu ya waliohudhuria msiba wa Sajuki katika makaburi ya Kisutu wakiwa wametulia huku kila mwenye kamera akijaribu kuchukua matukio.
Wadau mabali mbali wakisubiria mwili wa Marehemu Sajuki, huku Profesa Jay akionekana kwa mbali miongoni mwa wanaousubiri mwili ili shughuli ya mazishi iendelee.Wanahabari nao kama kawaida wakiwa na zana za kazi.

Umati wa watu ukiwa makaburini Kisutu Dar tayari kwa shughuli ya mazishi ya SAJUKI.
 Mwili wa marehemu Sajuki ukiwasili katika makaburi ya Kisutu tayari kwa mazishi huku wanahabari nao wakiwa wamenyanyua vitendea kazi vyao juu ili kuweza kupata matukio vizuri.
  Hapa ndipo sajuki amelala ndugu,jamaa na marafiki wakitengeneza vizuri Kaburi lake baada ya shughuli ya  kufukia.
  Source; Rundugai Blog

No comments: